Kutokana na ongezeko la matukio ya moto wa misitu na uharibifu wa rasilimali za asili nchini, Serikali imeelekeza kuimarishwa kwa elimu na uhamasishaji wa wananchi ili kuongeza ushiriki katika kulinda misitu, kudhibiti majanga ya moto na kuhamasisha uwekezaji endelevu katika sekta hiyo muhimu ya uchumi.