Mtaalamu asimulia alivyochunguza video ya Lissu kesi ya uhaini

Shahidi wa tatu wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesimulia mahakamani namna alivyofanya uchunguzi wa picha mjongeo (video clip) inayomuonesha Lissu akitamka maneno yanayodaiwa kuwa ya uhaini.