OMO aahidi kukomesha ufisadi taasisi nne Zanzibar ndani ya siku 100

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema akitangazwa kuwa rais wa kisiwa hicho, atafukua makaburi ili kushughulikia kile alichodai ni ubadhirifu wa uendeshaji katika taasisi nne.