Sh228 milioni zaboresha miundombinu ya Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya

Zaidi ya Sh228 milioni zimetumika kuboresha miundombinu ya jengo na vifaa muhimu katika wodi ya watoto wachanga ya Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, ikiwa ni hatua muhimu ya kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa njiti au wenye changamoto za kiafya.