Wananchi wapewa angalizo kubadili mfumo wa maisha kukabili matatizo ya kiafya

Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) limeitaka jamii kubadili mifumo ya maisha kwa kufanya mazoezi zaidi, kula kwa uangalifu na kujali afya ya akili, kama sehemu ya juhudi za kitaifa za kuwa na jamii yenye afya bora.