Waandishi wa habari Iringa waomba ulinzi wakifuatilia habari za rushwa
Waandishi wa habari mkoani Iringa wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhakikisha ulinzi na usalama wao, hasa wanaporipoti taarifa nyeti zinazohusu vitendo vya rushwa vinavyohusisha watu wa ngazi mbalimbali katika jamii.