Mgombea ubunge wa Jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Profesa Adolf Mkenda amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anaboresha Zahanati ya Kidale iliyopo Kata ya Katangara Mrere, ili ipandishwe hadhi na kuwa kituo cha afya cha mfano katika jimbo hilo.