SAU yailalamikia INEC mkanganyiko wa ratiba za kampeni, wenyewe wajibu

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara ameishutumu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kile alichokiita changamoto za uratibu wa ratiba za kampeni, hali ambayo amesema imekuwa ikisababisha mkanganyiko na migongano katika maeneo ya mikutano.