Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Othman Othman, amewapongeza maafisa na askari wa kikosi cha Polisi Jeshi waliomaliza jukumu lao la ulinzi wa amani nchini Lebanon. Ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akipokea bendera ya taifa kutoka kwa kikosi hicho, katika hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ulinzi wa Amani …