Wakulima Rungwe walalamikia wizi wa parachichi, watishia kukata miti

Wimbi la wizi wa parachichi shambani limeibua taharuki kwa wakulima wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, huku baadhi yao wakitishia kukata miti ya zao hilo na kuachana na kilimo hicho endapo Serikali haitachukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo.