Dk Nchimbi aitaka wizara ya maji kushirikiana na sekta binafsi kutatua changamoto ya maji

Makamu wa Rais Balozi, Dk Emmanuel Nchimbi ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maji kujenga ushirikiano na sekta binafsi ili kushughulikia changamoto za upatikanaji na upotevu wa maji, ili dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua “mama ndoo kichwani” iweze kutekelezeka.