Swahili Times
Madaktari sita wa Hospitali ya Sekou-Toure mkoani Mwanza wamejeruhiwa baada ya gari walilopanda aina ya Toyota Land Cruiser Hardrop kupata ajali Kijiji cha Maremwe Kata ya Igongwa wilayani Kwimba wakati wakitoka kutoa huduma kwenye kambi ya matibabu ya kibingwa katika Hospitali ya Icheja. Polisi mkoani humo wamesema chanzo cha ajali ni baada ya dereva kujaribu kumkwepa mpanda baiskeli aliyekuwa ameanguka barabarani. Aidha, majeruhi wawili wameruhusiwa huku wanne wakiendelea na matibabu. Majeruhi hao ni pamoja na Dkt. James Nkya (38), Dkt. Self Mmka (38), Dkt. Stanley Makundi (37), Dkt. Aretha Masawe (35), Dkt. Mary Urasa (27) na Dkt. Frank Mgeta (42). The post Madaktari 6 wajeruhiwa katika ajali Mwanza appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site