Collector
Nusura lofa afe akimfurahisha kipusa mpwani | Collector
Nusura lofa afe akimfurahisha kipusa mpwani
LA TAIFA LEO

Nusura lofa afe akimfurahisha kipusa mpwani

LOFA aliyetembelea Pwani kwa mara ya kwanza kutoka sehemu za bara aliokolewa yu mahututi baharini akijaribu kumridhisha binti wa kisiwani hapa aliyekuwa amemrushia mistari. Walioshuhudia wanasema jombi alikuwa amemtongoza binti huyo lakini akampa mtihani wa kuogelea kuelekea ndani ya bahari kiasi cha umbali wa mita hamsini hivi kutoka ufukweni na kurudi alikokuwa. Binti alimwahidi kuwa endapo angeupita mtihani huo basi atamkubali mzimamzima. Kwa tamaa aliyokuwa nayo, jamaa alijitosa baharini ghafla na baada ya dakika chache tu hivi alianza kupiga mayowe akizama na kuomba kuokolewa. Kwa bahati nzuri kulikuwa na wapigambizi wa kujitolea waliokuwa wakipiga doria ufukweni. Mara moja walijitosa ndani na kumuokoa lofa huyo. Hivyo ndivyo jombi wa kutoka bara alivyomkosa binti wa Kipwani.

Go to News Site