Collector
Jinsi ya kulima stroberi | Collector
Jinsi ya kulima stroberi
LA TAIFA LEO

Jinsi ya kulima stroberi

ANTHONY Ngatia, mkulima barobaro kutoka Kaunti ya Kiambu, amekuwa akikuza stroberi tangu mwaka 2024, na kuifanya matunda hayo kuwa chanzo chake kikuu cha mapato. Kwa muda, mkulima huyu anayeishi Mwihoko amebobea katika kilimo cha zao hili la bustani lenye thamani kubwa. Akiwa angali mkulima mdogo, anasema kuwepo na mipango mizuri, mbinu bora za kilimo, na matumizi ya teknolojia za kisasa, wakulima wanaweza kupata mavuno mengi hata katika mashamba madogo. Ngatia amekumbatia mfumo wa Artificial Intelligence (AI) kukabiliana na changamoto za kilimo, hasa katika kupata ushauri wa kitaalamu wa kilimo. Kilimo cha stroberi huanza kwa uzalishaji wa miche kupitia runners — matawi madogo yanayotoka kwenye mmea mama. Anaeleza, “Huweka matawi hayo kwenye vikombe vilivyojazwa udongo uliochanganywa na mbolea na virutubisho, ambapo huota mizizi ndani ya wiki mbili kabla ya kuhamishiwa shambani.” [caption id="attachment_186754" align="aligncenter" width="300"] Anthony Ngatia akikagua na kuelezea kuhusu mimea ya stroberi katika shamba lake lililoko Mwihoko, Kaunti ya Kiambu, Machi 31, 2026. Picha|Sammy Waweru [/caption] Kabla ya kupanda, shamba huandaliwa kwa kufanya uchunguzi na utafiti wa udongo na kuuboresha kwa kutumia mbolea asilia kama samadi, biochar na lime ya kilimo. Anatumia matuta yaliyoinuliwa na kufunikwa kwa karatasi ya kuzuia mnyauko ya maji (mulching paper) ili kuzuia maji kusimama, kuhifadhi unyevuunyevu, na kuweka matunda katika hali safi. Mfumo wa umwagiliaji wa matone hutumika kusambaza maji kwa kiwango kinachofaa, kwani stroberi huhitaji unyevu wa mara kwa mara lakini huathirika na maji mengi kupita kiasi. Kulingana na Richard Omondi, mwanzilishi wa Agri-Irrigation and Solutions Africa, mimea ya stroberi huchukua karibu miezi minne baada ya kupandikizwa kuanza kuzalisha matunda. “Katika kipindi hiki, lishe bora ni muhimu. Stroberi huhitaji virutubisho vingi, ikiwemo nitrojeni kwa ukuaji wa majani, na kalsiamu, potasiamu pamoja na virutubisho vinginevyo wakati wa kuchana maua na utoaji matunda,” anashauri. Kupogoa mara kwa mara, kudhibiti wadudu na magonjwa, pamoja na ufuatiliaji wa karibu, pia ni mambo muhimu katika kuhakikisha afya ya mimea na kuongeza mavuno. [caption id="attachment_186755" align="aligncenter" width="300"] Anthony Ngatia akivuna stroberi katika shamba lake lililoko Mwihoko, Kaunti ya Kiambu, Machi 31, 2026. Picha|Sammy Waweru [/caption] Kuna aina mbalimbali za stroberi zinazolimwa nchini Kenya, ambazo ni; Chandler, San Andreas na Douglas, ni miongoni mwa aina maarufu na zenye faida. Ngatia analima aina ya San Andreas kwenye kivungulio (greenhouse). Ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea bila kukatika, hupanda kwa awamu, aking’oa polepole mimea ya zamani au iliyoathiriwa na magonjwa kwa kuibadilisha na miche mipya. Baadhi ya mimea katika shamba lake ina umri wa hadi miaka miwili, huku mingine ikiwa na miezi michache tu. Mkulima huyo pia amekumbatia mifumo ya kilimo cha hydroponic — njia ya kilimo bila kutumia udongo ambayo inaweza kuongeza mavuno, kupunguza hatari ya magonjwa, na kuongeza kiwango cha uzalishaji hata katika nafasi ndogo.

Go to News Site