Collector
Jela miezi 6 kwa kuzusha kuibiwa nyeti Geita | Collector
Jela miezi 6 kwa kuzusha kuibiwa nyeti Geita
Swahili Times

Jela miezi 6 kwa kuzusha kuibiwa nyeti Geita

Mahakama ya Mwanzo Nyankumbu, wilayani Geita mkoani Geita imemhukumu kifungo cha miezi sita jela Abdulazizi Kabangila (31), mkazi wa Mwatulole kwa kutoa taarifa za uongo kuwa amepoteza nyeti zake baada ya kuguswa bega na Veradius Magogo. Mahakama imeeleza kuwa mshtakiwa kwa kushirikiana na wananchi, walimshambulia Magogo na kumsababishia maumivu makali mwilini, akihamasisha kundi la watu kutaka kujichukulia sheria mkononi.  Hata hivyo, uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na madaktari kutoka Hospitali ya Serikali ulithibitisha pasi na shaka kuwa madai ya mshitakiwa yalikuwa ni ya uongo na upotoshaji, kwani viungo vyake vilikutwa vikiwa katika hali ya kawaida ya kimaumbile. The post Jela miezi 6 kwa kuzusha kuibiwa nyeti Geita appeared first on SwahiliTimes .

Go to News Site