Swahili Times
Muungano wa watoa huduma za mawasiliano nchini (Telco Operators Consortium) umekamilisha rasmi ujenzi wa minara ya mawasiliano 758 na kukabidhi zaidi ya kilomita 1,100 za miundombinu ya nyaya za fiber optic kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatua ambayo ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mpango wa taifa wa kupanua miundombinu ya mawasiliano. Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Mradi huo umejengwa kupitia ushirikiano wa muda mrefu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), ukiwa na lengo la kuharakisha upatikanaji wa […] The post Yas Tanzania yaongoza Muungano wa Watoa huduma za Mawasiliano kukabidhi miundombinu ya Mawasiliano Serikalini appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site