LA TAIFA LEO
MANYANI, Tsavo: SAFARI ya kuelekea Mombasa ya kikundi cha akina mama nusura ikatike basi lilipokwama kutokana na kile kilichogunduliwa kuwa nguvu za ndumba za mmoja wao. Inasemekana kuwa basi hilo lilisimama katikati ya pori bila sababu. Dereva alijaribu kuwasha mara kadhaa bila mafanikio. Abiria walianza kunong’ona kila mmoja akimtazama jirani yake kwa shaka. “Hii si kawaida, kuna ndumba hapa,” mmoja wao alisema baada ya kuomba kwa dakika chache na kuchochea wenzake waliotaka aliyehusika na hirizi kuzitupa. Inasemekana mmoja wao alitoka na mkoba wake huku wenzake wakimtazama akachomoa mifupa mitatu na kuitupa porini kisha gari likawaka na safari ikaendelea.
Go to News Site