Collector
Trump sasa asema iwapo Iran inataka mazungumzo ‘impigie simu’ | Collector
Trump sasa asema iwapo Iran inataka mazungumzo ‘impigie simu’
LA TAIFA LEO

Trump sasa asema iwapo Iran inataka mazungumzo ‘impigie simu’

WASHINGTON/Islamabad: RAIS Donald Trump amesema Iran inaweza kuwasiliana kwa njia ya simu ikitaka kuendelea na mazungumzo ya kukomesha vita ambavyo vimedumu kwa miezi miwili huku akisisitiza kuwa Iran inafaa kuzima mpango wake wa nyuklia. Rais huyo wa Amerika alisema hayo baada ya Iran kusema nchi hiyo inapaswa kuondoa vikwazo katika kuafikiwa kwa makubaliano, ikiwemo vizuizi ilivyoweka katika bandari za Iran. Iran imekubali kufungua Mkondo wa Hormuz pasi kushughulikia suala la mpango wake wa nyuklia, maafisa wawili wa ukanda wa Mashariki ya Kati wenye ufahamu kuhusu pendekezo hilo walisema jana. Matumaini ya kurejelewa kwa juhudi za kurejeshwa kwa amani yalififia Jumatano baada ya Rais Trump kuzima safari ya mabalozi wake Steve Witkoff na Jared Kushner ya kuelekea jijini Islamad, Pakistan. Naye Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi jana alielekea Urusi baada ya kuingia na kutoka nchi za Pakistan na Oman, zinazosimamia mazungumzo hayo. Aliwasili katika Saint Petersburge Jumatatu, Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Iran ilisema kupitia mtandao wa Telegram. Waziri Araghchi alitarajiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Mkutano Wakati wa mkutano huo, majadiliano yatahusu uhusiano kati ya Iran na Urusi, vita vya Iran na Amerika, miongoni mwa masuala mengine ya ukanda wa Mashariki ya Kati, alisema Waziri Araghchi. Waziri huyo alisema kwamba mazungumzo ya hivi majuzi nchini Pakistan yamebadilisha masharti yatakayozingatiwa kurejesha mazungumzo kati ya Iran na Amerika, akisisitiza kuwa Iran itatetea haki zake na maslahi ya kitaifa kufuatia kutokea kwa vita hivyo vilivyodumu kwa miezi miwili. Araghchi aliongeza kuwa Iran na Oman, kama mataifa yanayopakana na Mkondo wa Hormuz, yamekubaliana kuendeleza mazungumzo ya kitaalamu kuhakikisha usalama wa vyombo vya usafirishaji bidhaa na kulinda maslahi yao katika njia hiyo ya baharini.

Go to News Site