Swahili Times
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni kuwa Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani alipigwa makofi na mwanajeshi katika eneo la Msamvu. Polisi wamesema tukio hilo limebuniwa kwa lengo la kupotosha umma na kuchafua taswira ya vyombo vya ulinzi na usalama. Aidha, Polisi wametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kueneza tabia za upotoshaji kwa jamii, kwani halitasita kuchuakua hatua kali dhidi yao. The post Polisi wakanusha Askari kupigwa makofi na mwanajeshi appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site