Swahili Times
Jeshi la Polisi limesema limewakamata watuhumiwa watatu wanaodaiwa kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kutoa matusi kwa wengine wakiwemo wajumbe wa Tume ya uchunguzi wa ghasia za Oktoba 2025. Polisi wamesema watuhumiwa hao wamekamatwa mikoa ya Arusha, Iringa na Mbeya huku msako wa kuwakamata wengine ukiendelea. “Msako wa kuwakamata wengine bado unaendelea ikiwemo wale ambao waliotumiwa na wahalifu hao jumbe za matusi, kudhalilisha, kashfa, uchonganishi, kupandikiza chuki na upotoshaji na wao wakaendelea kizisambaza,” imesema taarifa ya Polisi. Aidha, Polisi wamesema taratibu za kisheria zinaendelea kwa watuhumiwa. The post Watatu wakamatwa kwa kuwatuma wajumbe wa Tume appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site