Collector
Wanne wakamatwa kwa kujaribu kuiba mafuta ya ndege | Collector
Wanne wakamatwa kwa kujaribu kuiba mafuta ya ndege
Swahili Times

Wanne wakamatwa kwa kujaribu kuiba mafuta ya ndege

Watu wanne, wanaume watatu na mwanamke mmoja, wamekamatwa wakijaribu kuiba mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi nchini Kenya. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) amesema kukamatwa kwao kulifanywa na maafisa wa Kitengo cha Polisi wa Viwanja vya Ndege (KAPU), baada ya polisi kubaini shughuli za kushuku katika gari walilokuwa wakitumia. Washukiwa hao waliokuwa kwenye gari aina ya Mitsubishi Canter walikamatwa wakiwa katika jaribio la kutoa lita 800 za mafuta kutoka kwenye ndege iliyokuwa uwanjani hapo. The post Wanne wakamatwa kwa kujaribu kuiba mafuta ya ndege appeared first on SwahiliTimes .

Go to News Site