Swahili Times
Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania, kwa kushirikiana na Bilal Muslim Mission of Tanzania pamoja na KSI Charitable Centre, imeendesha kambi ya siku tatu ya huduma za macho bure kwa wananchi wa Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi. Kupitia kambi hiyo, mamia ya wananchi walipata huduma mbalimbali ikiwemo vipimo vya macho, matibabu pamoja na upasuaji wa macho uliotekelezwa na madaktari bingwa. Lengo la mpango huo ni kusaidia jamii kupata huduma za afya ya macho kwa urahisi, hususan kwa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu. Akifungua rasmi kambi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo, aliwataka wazazi kuchukua […] The post Yas Tanzania Yaendesha Kambi ya Huduma za Macho Bure Kilwa appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site