Swahili Times
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa mitandaoni ikieleza kuwa gari inayodhaniwa kuwa ni ya kubeba wagonjwa (ambulance) ilimtelekeza mwanaume akiwa amefariki eneo la Mbwaruki, Wilaya ya Moshi. Taarifa iliyotolewa na polisi imesema uchunguzi wa awali unaeleza kuwa Mei 6, 2026 majira ya saa moja jioni, Ismail Amani Mbowe (33), mkazi wa Machame akiwa anaendesha pikipiki (MC 336FHV) alipata ajali eneo la Uchira Karamsingi baada ya kugonga gari (T974EHQ/T947EJN) aina ya Howo. “Wananchi walikusanyika na kutoa msaada wa awali kabla ya polisi kufika eneo hilo, kwa kuomba msaada kwenye gari iliyotajwa kuwa ni gari ya wagonjwa […] The post Polisi: Tunachunguza ‘Ambulance’ kumtelekeza majeruhi appeared first on SwahiliTimes .
Go to News Site