LA TAIFA LEO
MWANIAJI wa kiti cha ubunge cha Emurua Dikirr kwa tikiti ya UDA David Kipsang Koech amechukua uongozi wa mapema kura zikiendelea kuthibitishwa na kuhesabiwa na IEBC. Kufikia 1.11am, David Koech anayefahamika maarufu kama Dollarline alikuwa anaongoza kwa kura 11,643 huku mpinzani wake mkuu, Vincent Rotich almaarufu ‘Pinceent’ wa DCP alikuwa na kura 7,839. Kura hizi zilitokana na vituo 64 kati ya 94 vilivyokuwa vimehesabu kura kufikia muda huo.
Go to News Site