Collector
Watafiti waonya hatari ya wanaume kurudia vazi la ndani bila kuosha | Collector
Watafiti waonya hatari ya wanaume kurudia vazi la ndani bila kuosha
LA TAIFA LEO

Watafiti waonya hatari ya wanaume kurudia vazi la ndani bila kuosha

MWANAMUME mmoja kati ya watano hurudia kuvaa chupi aliyoivaa siku iliyopita, watafiti wamebaini. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha New York, pia walibaini kuna uwezekano kuwa wiki haitaisha kabla ya mwanaume kurudia chupi aliyovaa jana au leo. Katika hali ya kushangaza, kuna kundi la wanaume ambao huvaa chupi moja wiki nzima bila kuibadilisha na hawajali. Mtafiti kutoka Chuo hicho, Dkt Philip Tierno aliafikia hilo baada ya kuwashirikisha wanaume na wanawake 2,000 kwenye utafiti wake. Asilimia 45 ya watu hao walikiri kuwa huwa wanarudia kuvaa chupi kwa siku mbili zinazofuatana. Hata hivyo, kulikuwa na tofauti kubwa kati ya wanaume na wanawake. Hii ni kwa sababu wanaume walipatikana wanarudia chupi mara mbili na nusu zaidi kuliko wanawake kwa wiki moja au hata siku nyingi zaidi. Hali hii ni hatari kwa mujibu Dkt Tierno, ambaye pia ni Profesa katika masuala ya bakteria katika chuo hicho cha New York. Mtaalamu huyo, anasema kuwa hata chupi ambazo zimeoshwa zinaweza kuwa na maelfu ya bakteria baada ya kuvaliwa mara moja. “Kuvaa chupi moja kwa muda mrefu huchangia kurundikana kwa bakteria, kuchipuka kwa magonjwa ya ngozi na pia chupi zenyewe huwa na harufu kali kutokana na uchafu,” akasema Dkt Tierno. Utafiti huo pia ulifichua kuwa asilimia 46 ya watu huwa wanaweza kutumia chupi moja nyakati tofauti na kusalia nayo kwa mwaka moja au zaidi. Hii ina maana kuwa wengi hawamakinikii kununua chupi na hata wakizinunua, huwa nazo kwa mwaka mmoja na zaidi. Wengine hata zikizeeka na kuchakaa bado huzivaa tu kwa kuwa zinafunikwa na long’i. “Wakati mwingine mambo madogo ambayo hutuathiri ndiyo sisi hupuuza sana. Hili la chupi linahitaji umakinifu zaidi,” akasema mtaalamu huyo.

Go to News Site