LA TAIFA LEO
TAKRIBAN wanafunzi 15 wameripotiwa kufariki katika mkasa wa moto uliotokea katika shule ya Utumishi Girls iliyoko Gilgil, Kaunti ya Nakuru. Ripoti ya polisi inasema kwamba moto huo uliripotiwa saa saba za usiku katika bweni la wanafunzi 220 wa Gredi ya 10, Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne. Inasema juhudi za kuzima moto zilizoongozwa na zimamoto wa Naivasha, KDF, Idara ya Misitu na NYS zilisaidia kukabili moto huo ingawa tayari maafa yalikuwa yametokea huku idadi isiyojulikana ya waliojeruhiwa wakikimbizwa katika hospitali mbali mbali. Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…
Go to News Site