LA TAIFA LEO
ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua amepata pigo kubwa mahakamani, baada ya jopo la majaji watatu kutupilia mbali kesi ya kupinga kutimuliwa kwake serikalini. Katika uamuzi wa majaji Fridah Mugambi, John Mrima na Eric Ogola, walisema kwamba sheria zilifuatwa katika mchakato mzima wa kumtimua Bw Gachagua uongozini. Mahakama ilikuwa imeorodhesha malilio sita ya Gachagua ambayo mawakili wake waliwasilisha wakitaka uamuzi bayana kuyahusu. Nayo yalikuwa iwapo Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kisheria kusikiza kesi yake, kwamba kulikuwa na uonevu dhidi yake, iwapo umma ulihusishwa katika kutoa maoni, uhalali wa kanuni za bunge zilizotumiwa katika mchakato wa kumtimua, ufaafu wa Kindiki kuchukua wadhifa wake na iwapo Katiba ilifuatwa katika kumtimua.
Go to News Site