Huzuni mvulana wa miaka 14 akiuawa na simba eneo la Marafa akitoka shuleni
LA TAIFA LEO

Huzuni mvulana wa miaka 14 akiuawa na simba eneo la Marafa akitoka shuleni

FAMILIA katika eneo la Marafa, Kaunti ya Kilifi, inataka haki itendeke baada ya mwana wao kuuawa na simba akitoka shuleni. Simion Nzaro Chai, 14, alikosa kurudi nyumbani Jumanne jioni na mwili wake ukapatikana Jumatano kichakani ukiwa bila baadhi ya sehemu. Babake, Bw Jackson Nzaro Chai, alitaka serikali iwajibike kuhusu kisa hicho, huku wakazi wakisema wamekuwa wakilalamikia uvamizi wa wanyamapori kwa muda mrefu bila hatua zozote kuchukuliwa. Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Magarini Francis Mwangi, alisema kikosi cha maafisa kutoka vitengo mbalimbali wakiwemo wa Shirika la Kuhifadhi Wanyamapori (KWS) kimetumwa kumtafuta simba huyo. Alisema akipatikana atarudishwa mbugani au hata kuuawa. Walimu walilalamika kuwa wamelazimika kuruhusu watoto kuchelewa kuingia shuleni na kurudi nyumbani mapema kwa muda mrefu sasa kwa sababu wanahofia wanaweza kushambuliwa na wanyamapori wanaotoka mbuga ya Tsavo.

Go to News Site