Collector
Giriş Yap
Jinsi ya kujibu maswali ya Fasihi Simulizi | Collector
Jinsi ya kujibu maswali ya Fasihi Simulizi

Jinsi ya kujibu maswali ya Fasihi Simulizi

SOMA hadithi ifuatayo kisha jibu maswali. Mababu zetu waliturithisha heshima, utu, utamaduni imani na upendo. Tunatambua nia yao njema ya kuona jamii ikiishi kwa utulivu, umoja, mshikamano na uelewano. Leo hii nyuso zetu zimesawijika. Nyuso zimeinama kwa matokeo mabaya ya kitendo cha ubinafsi, unyama na ukatili cha mmoja wetu. Kama jamii, kama watu wa ukoo wa Shani wa Miramba, tunajitenga na ila hii. Tunamkana Kaliko wa Ndaya. Damu yake si yetu. Tunakemea na kulaani kitendo chake cha ubakaji. Tunalaani umaluuni huu kwa kinywa kipana. Mababu zetu wamemkataa. Mungu wetu mwenye kutaka heri kwa waja wote atuepushe adhabu na ghadhabu yake. Tunaomba dua kwako Mungu wa Mlima mkuu uliovikwa kofia ya theluji na kutukuka. Yalinde mashamba yetu tupate mazao mazuri; ila iliyoingia kwetu isije na kiangazi. Mawindo ya usasi wetu yasitupotelee kutokana na kasoro hii. Tunaomba mito yetu isikauke tusikose kitoweo humo na maji kwa mifugo wetu. Bariki ukoo wetu mtukuka. Tubaki imara kama mwamba. Ukoo wetu ni nyota siku zote. Ndiyo ni nyota! Ukoo wa Shani wa Miramba udumu milele! a) Bainisha kipera cha utungo huu Maapizo - Kuna maombi maalum kuiepusha jamii na laana kutokana na kitendo cha ubakaji. b) Taja sifa zozote tano za kipera hiki Hutolewa dhidi ya walioenda kinyume na matarajio ya jamii. Maombi huelekezwa kwa Mungu, miungu au mizimu. Hutolewa na watu maalum kwenye jamii kama vile wazee, viongozi wa kidini, n.k. Huwa na lugha ya kutisha na kutia uoga. Aliyetenda uovu huelekezewa laana na mikosi. Huweza kutolewa kabla ya kula viapo. Huwasilishwa mahali maalum kama vile, chini ya miti ‘mitakatifu’, mapangoni, maeneo ya ibada, kando ya mito Huweza kuandamana na kafara kwa miungu au mizimu. Kwa baadhi ya jamii, huwasilishwa wakati maalum kama vile, asubuhi na mapema, jioni. Wakati mwingine, aliyeenda kinyume na jamii huhitajika kutoa zawadi kwa mizimu ili asamehewe / atakaswe. Huwa na masharti makali yanayoelekeza namna ya kutolewa, wanaoshiriki na njia ya kutenda vitendo vinavyoandamana na maapizo. Huandamana na matendo maalum kama vile, kuinua mikono, kutazama juu, kuinamia sehemu fulani maalum, kupiga magoti n.k Kwa baadhi ya jamii kigezo cha umri au jinsia huzingatiwa kwa wanaoshiriki kuwasilisha maapizo k.m wazee wa kiume wa umri fulani (wakongwe) c) Mwasilishaji wa kipera hiki anahitajika kuwa na wasifu upi ili kukifanikisha? Mjuzi wa lugha / awe mlumbi bora. Atumie lugha fasaha. Awe na umri unaofaa. Katika jamii nyingi, maapizo huwasilishwa na wazee. Fanani awe na nafasi/hadhi ifaayo katika jamii husika, kama vile, viongozi wa kidini ama watu maalum walioteuliwa katika jamii. Wakati mwingine avae maleba maalum yanayohitajika k.v mavazi ya kidini Sauti kakamavu na inayosikika vizuri. Aweze kutumia ishara na miondoko inayohitajika. Awe na uelewa mzuri wa utamaduni wa jamii husika.

Go to News Site