Mambo yako shwari sasa JKIA- KAA yasema

Mambo yako shwari sasa JKIA- KAA yasema

SHUGHULI za kawaida zimerejea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) baada ya kusitishwa kwa muda mapema Alhamisi Oktoba 16, 2025. Kwenye taarifa mwendo wa saa nane alasiri, Mamlakaya Kusimamia Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) ilithibitisha kuwa safari za ndege zimerejelea kama kawaida na kuwahakikishia wananchi kwamba usalama umewekwa. “Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) sasa umefunguliwa kwa shughuli za kawaida baada ya kufungwa kwa muda mapema leo (Alhamisi),” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa KAA Mohamud Gedi akasema. Aliwashauri wasafiri, ambao safari zao zilikuwa zimeratibiwa wakati shughuli zilipositishwa, kuwasiliana na mashirika husika ya ndege kwa maelezo kuhusu safari zao. KAA iliwashukuru wasafiri, mashirika ya safari za ndege na umma kwa ujumla kwa uvumilivu wao wakati shughuli zilisitishwa kwa muda katika JKIA. “Tumejitolea kutoa huduma bora za usafiri na huduma nyinginezo katika JKIA kwa njia bora,” Bw Gedi akaeleza. Awali, majira ya asubuhi, Mamlaka ya Kusimamia Safari za Angani (KCAA) ilisitisha shughuli kwa muda katika uwanja wa JKIA baada ya waombolezaji kuvuruga usalama humo wakati kuwasili kwa mwili wa Hayati Raila Odinga. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari mamlaka hiyo ilisema ililazimika kuchukua hatua hiyo baada ya waomboleza kuingia sehemu zisizoruhusiwa katika uwanja huo. “KCAA inajulisha umma kwamba shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta zimesitishwa kwa muda kutokana na hali ya usalama iliyoshughuhiwa kufuatia kuwasilisha kwa mwili wa Mheshimiwa Raila Odinga,” akasema Mkurugenzi Mkuu wa KACC Emile Arao. Mamlaka hiyo ilitoa wito kwa umma na wasafiri kusalia watulivu na kutofika katika uwanja huo wa ndege hadi mwelekeo utakapotolewa baadaye. “Shughuli za kawaida zitarejelewa kama kawaida baada ya uwanja wa JKIA kutawazwa kuwa salama,” Bw Arao akasema. Ndege ya Shirika la Ndege Nchi (KQ)  iliyobeba mwili wa Raila ilipowasili katika uwanja huo, maelfu ya waombolezaji walionekana kuwalemea maafisa wa vikosi mbalimbali vya usalama. Isitoshe, baadhi yao, waliokuwa wakilia kwa sauti wakibeba matawi, walionekana karibu zaidi na ndege hiyo iliyopewa jina “RAO OO1”.

Prince Indah atoa wimbo wa kumwomboleza Raila

Prince Indah atoa wimbo wa kumwomboleza Raila

MWANAMUZIKI maarufu Evans Ochieng Owino anayefahamika sana kama Prince Indah ametoa wimbo mpya wa kumwomboleza Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga. Kupitia wimbo huo Tribute to RT. Hon Raila Odinga alioutoa saa saba zilizopita, Indah anamsifu sana Bw Odinga huku akimrejelea kama shujaa ambaye ameleta mabadiliko makubwa nchini. “Apenjo, kara iwewa gi ng’awa, dwoka kiwinja Baba (Nauliza, unatuacha na nani Baba, naomba unijibu ikiwa unanisikiza),” Indah anasema katika wimbo huo. Kwa upande mwingine, mwanamuziki huyo mashuhuri anasema kuwa Bw Odinga alileta demokrasia nchini na kupigania haki za wanyonge. “Kata Gen-Z bende yuaka (Hata vijana wa Gen Z wanaomboleza kifo chako).” “Piny yuak. Kata ka Nyasaye otimo dwache, matolit jothurwa (Dunia inaomboleza. Habari hii inauma).” Watu zaidi ya 164,651 wamesikiza wimbo huo. Indah ameonekana mara kadhaa akiwa na Bw Odinga wakifurahia nyimbo za mwanamuziki huyo. Bw Odinga alifariki dunia Jumatano asubuhi Oktoba 15, 2025 huko Koothattukulam, wilayani Ernakulam nchini India, baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati anafanya matembezi yake ya kila asubuhi, kulingana na polisi na viongozi wa hospitali. [caption id="attachment_179232" align="alignnone" width="300"] Raila Odinga ambaye aliaga dunia Oktoba 15, 2025. Picha|Maktaba[/caption] Odinga, mwenye umri wa miaka 80, aliangua wakati wa matembezi ya asubuhi ndani ya uwanja wa kituo cha tiba ya Ayurveda, na alikimbizwa Hospitali ya Macho ya Sreedhareeyam Ayurvedic na Kituo cha Utafiti huko Koothattukulam, ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia, msemaji wa hospitali hiyo alisema. Kando na Indah, wanamuziki wengi akiwemo Bahati wametoa nyimbo za kumwomboleza Bw Odinga wakimtaja kama kiongozi mashuhuri na mtetezi wa demokrasia. Katika miaka ya hivi karibuni, Indah ameinuka kwa kiwango kikubwa katika tasnia ya muziki. Alianza kuimba kwenye bendi ya R.O.R iliyokuwa ikimilikiwa na Emma Jalamo kabla ya kuwa msanii huru. Mwaka 2014 alirekodi albamu yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 6 ambazo ni pamoja na Cinderella, Nyakisumu, Pokna, Uchumi na Ken Soldier. Oktoba 2016, Prince Indah alirekodi albamu ya pili aliyoipa jina ‘Tenda Wema’ aliyozindua rasmi Desemba 23 mwaka huo. Baada ya hapo aliondoka kwenye bendi ya R. O. R na kuunda yake Malaika Ohangla Rhumba – M.O.R.

Chaos at Kasarani as Police Disperse Mourners with Tear Gas

Chaos at Kasarani as Police Disperse Mourners with Tear Gas

Police on Thursday afternoon fired tear gas at Moi International Sports Centre, Kasarani, dispersing thousands of mourners who had gathered to view the body of former Prime Minister Raila Amolo Odinga. The situation quickly turned chaotic as thick clouds of tear gas filled the 48,000-capacity stadium, forcing mourners to flee in panic. Within minutes, the [...] The post Chaos at Kasarani as Police Disperse Mourners with Tear Gas appeared first on Kahawatungu .