US says working on new $20 bn 'facility' for Argentina

US says working on new $20 bn 'facility' for Argentina

US Treasury Secretary Scott Bessent on Wednesday said he was working to help corral the private sector around a new $20 billion "facility" to support Argentina's embattled economy. Bessent added that he had spent "weeks" working on the private-sector solution to Argentina's upcoming debt payments, which would come on top of the $20 billion US swap line the US Treasury recently set up.

Raila Odinga aombolezwa na wanamichezo, alipenda soka sana

Raila Odinga aombolezwa na wanamichezo, alipenda soka sana

WANAMICHEZO nchini Kenya wanaomboleza kifo cha mmoja wa wafuasi wakubwa wa michezo, Raila Amolo Odinga mnamo Jumatano, Oktoba 15, 2025. Kiongozi huyo mashuhuri anayejulikana kwa majina kama Tinga, Baba, RAO, na Agwambo, alikuwa shabiki mkubwa wa Gor Mahia, Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza na pia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars. Odinga aliaga dunia nchini India alipokuwa akipokea matibabu. Ripoti kutoka India zinasema alizimia wakati wa matembezi ya asubuhi na kufariki. Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limesema linaungana na taifa kuomboleza kifo cha Mheshimiwa Odinga. “Alikuwa kiongozi mwenye maono na shabiki wa kweli wa kandanda ya humu nchini. Urithi wake utaendelea kuhamasisha vizazi vijavyo. Tunatuma rambirambi zetu kwa familia yake, marafiki, na Wakenya wote katika wakati huu mgumu,” FKF inayoongozwa na Hussein Mohammed, ilisema. Shirikisho la Raga la Kenya (KRU) pia limesema: “Jumuiya ya raga inaungana na taifa kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga. Tunatuma salamu za pole kwa familia yake na Wakenya wote. Mchango wake katika kuijenga Kenya yenye umoja na maendeleo unabaki kuwa mwanga kwetu sote. Kama jamii ya raga, tunaheshimu urithi wake wa uongozi na uzalendo.” Klabu ya Gor Mahia, ambayo Odinga alikuwa mlezi wake kwa miaka 20, imemuomboleza ikisema: “Mioyo yetu imejaa huzuni kufuatia kifo cha mlezi wetu mpendwa, Mheshimiwa Raila Odinga. Alikuwa nguzo na mwanga kwa klabu yetu. Tunatuma rambirambi kwa familia yake. Pumzika kwa amani Baba.” Mahasimu wa tangu jadi wa Gor, AFC Leopards nao wamehuzika na kifo cha kiongozi huyo aliyesaidia klabu hizo mara kadhaa kifedha. “Kiongozi shupavu na shabiki mkubwa wa kandanda. Pumzika kwa amani Mheshimiwa Raila Odinga,” Leopards ikasema. Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, amesema taifa limepoteza nguzo kubwa ya uongozi. “Raila alikuwa mtu mwenye ujasiri, maono, na imani isiyotetereka katika demokrasia ya Kenya. Natoa rambirambi zangu kwa Mama Ida Odinga, familia ya Odinga, marafiki, na Wakenya wote. Raila alikuwa mwalimu kwa wengi, akiwemo mimi, na alijitolea kupigania ugatuzi, usawa, na taifa lenye umoja. Urithi wake wa uvumilivu, kujitolea na uzalendo utaendelea kuongoza safari ya kidemokrasia ya Kenya. “Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.”

Raila Odinga aombolezwa na wanamichezo, alipenda soka sana

Raila Odinga aombolezwa na wanamichezo, alipenda soka sana

WANAMICHEZO nchini Kenya wanaomboleza kifo cha mmoja wa wafuasi wakubwa wa michezo, Raila Amolo Odinga mnamo Jumatano, Oktoba 15, 2025. Kiongozi huyo mashuhuri anayejulikana kwa majina kama Tinga, Baba, RAO, na Agwambo, alikuwa shabiki mkubwa wa Gor Mahia, Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza na pia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars. Odinga aliaga dunia nchini India alipokuwa akipokea matibabu. Ripoti kutoka India zinasema alizimia wakati wa matembezi ya asubuhi na kufariki. Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limesema linaungana na taifa kuomboleza kifo cha Mheshimiwa Odinga. “Alikuwa kiongozi mwenye maono na shabiki wa kweli wa kandanda ya humu nchini. Urithi wake utaendelea kuhamasisha vizazi vijavyo. Tunatuma rambirambi zetu kwa familia yake, marafiki, na Wakenya wote katika wakati huu mgumu,” FKF inayoongozwa na Hussein Mohammed, ilisema. Shirikisho la Raga la Kenya (KRU) pia limesema: “Jumuiya ya raga inaungana na taifa kuomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga. Tunatuma salamu za pole kwa familia yake na Wakenya wote. Mchango wake katika kuijenga Kenya yenye umoja na maendeleo unabaki kuwa mwanga kwetu sote. Kama jamii ya raga, tunaheshimu urithi wake wa uongozi na uzalendo.” Klabu ya Gor Mahia, ambayo Odinga alikuwa mlezi wake kwa miaka 20, imemuomboleza ikisema: “Mioyo yetu imejaa huzuni kufuatia kifo cha mlezi wetu mpendwa, Mheshimiwa Raila Odinga. Alikuwa nguzo na mwanga kwa klabu yetu. Tunatuma rambirambi kwa familia yake. Pumzika kwa amani Baba.” Mahasimu wa tangu jadi wa Gor, AFC Leopards nao wamehuzika na kifo cha kiongozi huyo aliyesaidia klabu hizo mara kadhaa kifedha. “Kiongozi shupavu na shabiki mkubwa wa kandanda. Pumzika kwa amani Mheshimiwa Raila Odinga,” Leopards ikasema. Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, amesema taifa limepoteza nguzo kubwa ya uongozi. “Raila alikuwa mtu mwenye ujasiri, maono, na imani isiyotetereka katika demokrasia ya Kenya. Natoa rambirambi zangu kwa Mama Ida Odinga, familia ya Odinga, marafiki, na Wakenya wote. Raila alikuwa mwalimu kwa wengi, akiwemo mimi, na alijitolea kupigania ugatuzi, usawa, na taifa lenye umoja. Urithi wake wa uvumilivu, kujitolea na uzalendo utaendelea kuongoza safari ya kidemokrasia ya Kenya." “Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.”

Francesco Bagnaia Siblings: Meet Carola and Filippo Bagnaia

Francesco Bagnaia Siblings: Meet Carola and Filippo Bagnaia

Francesco “Pecco” Bagnaia is an Italian professional motorcycle racer, born on January 14, 1997, in Turin, Italy. At 28 years old, he has established himself as one of the premier talents in the MotoGP World Championship, riding for the Ducati Lenovo Team. Known for his aggressive braking style, precision in corners, and composure under pressure, [...] The post Francesco Bagnaia Siblings: Meet Carola and Filippo Bagnaia appeared first on Kahawatungu .

Wabunge kumwomboleza Raila mnamo Alhamisi, Spika Wetangula akiwataka wavalie mavazi meusi

Wabunge kumwomboleza Raila mnamo Alhamisi, Spika Wetangula akiwataka wavalie mavazi meusi

WABUNGE mnamo Alhamisi, Oktoba 16, 2025 watapata nafasi ya kumwombolewa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga aliyefariki Oktoba 15, akipokea matibabu nchini India. Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula Jumatano aliwaagiza wabunge kuvalia mavazi meusi akiwaambia “mje mkiwa na sura za huzuni”. “Napendekeza kwamba sote tuvalie mavazi meusi katika kikao hicho kitakachoanza saa nne asubuhi. Kwa wale ambao hawana mavazi meusi, tafadhali myanunue baada ya kikao hiki. Nao wenzetu wa kike waje na riboni kuashiria maombolezo,” akasema. “Katika kikao hicho, kila mbunge atapata nafasi ya kumwomboleza Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga baada ya habari kuhusu kifo chake kutangazwa rasmi na Rais William Ruto. Sote tuwe na sura ya maombolezo,” Bw Wetang’ula akaeleza. Spika, pia, aliamuru kwamba kikao cha alasiri cha bunge la kitaifa Alhamisi kitaanza saa nane na nusu hadi usiku wa manane (saa sita za usiku). Bw Wetang’ula alimtaja Raila kama kiongozi ambaye sifa zake zilizagaa kote nchini ambako alikuwa na wafuasi. “Waziri Mkuu wa zamani alikuwa mkubwa kuliko Kisumu. Alihusudiwa kuanzia Vanga hadi Lodwar. Na sifa zake zilienea hata nje ya mipaka ya taifa la Kenya,” akasema. Kiongozi wa Wengi, Kimani Ichung’wah aliwasilisha rasmi hoja ya kuahirishwa kwa kikao cha Jumatano ili kutoa nafasi kwa wabunge kuomboleza Hayati Mzee Odinga, kiongozi wa ODM. Hoja hiyo iliungwa mkono na kiongozi wa wachache Junet Mohamed ambaye alionekana kujawa na huzuni. Kufuatia kuahirishwa kwa kikao cha Alhamisi, mjadala kuhusu miswada kadhaa ilisitishwa. Baadhi ya miswada hiyo ni: Mswada wa Pareto, Mswada wa Huduma za Maktaba ya Kitaifa ya 2024, Mswada Kuhusu Afya ya Watoto Wachanga na Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Sekta ya Majani Chai.