How Ramón Ramírez Increased His Net Worth

How Ramón Ramírez Increased His Net Worth

Ramón Ramírez, a celebrated Mexican retired soccer player, has built an impressive career both on and off the field. With an estimated net worth of $2 million, Ramírez’s wealth reflects years of dedication, discipline, and passion for football. Born on December 5, 1969, in Tepic, Nayarit, Mexico, Ramírez became one of Mexico’s most admired midfielders [...] The post How Ramón Ramírez Increased His Net Worth appeared first on Kahawatungu .

Afisa aliyeuawa Ikulu Matanka na mshukiwa Kimunyi walikuwa marafiki, uchunguzi wabaini

Afisa aliyeuawa Ikulu Matanka na mshukiwa Kimunyi walikuwa marafiki, uchunguzi wabaini

RAMADHAN Matanka, 30, aliyeuawa akilinda Ikulu ya Nairobi Jumatatu, alikuwa tayari amewahudumia Marais wawili tofauti wa Kenya katika nyadhifa tofauti, kwa kipindi cha miaka mitatu. Matanka alipata kazi yake ya kwanza Ikulu mnamo mwaka wa 2020. Baba yake, Hassan Dabie Matanka, alikuwa mfanyakazi wa Ikulu. Rais wa wakati huo, Uhuru Kenyatta, alitoa agizo kuwa watoto wa wafanyakazi wa Ikulu waliokuwa wametimu umri wa miaka 18 waajiriwe katika mradi wa kusafisha Mto Nairobi na kusaidia katika usimamizi wa taka jijini. Kazi ya kwanza ya wafanyakazi waliofahamika kama Green Army ilikuwa kusafisha Ikulu vizuri – na ilikuwa pia njia ya kuwakinga vijana hao dhidi ya athari mbaya za mitaani. Wakati huo, Matanka alikuwa amemaliza mtihani wake wa KCSE. Vyanzo kadhaa vya karibu na uchunguzi wa mauaji ya kikatili ya Matanka vilifichua kuwa alikutana na Kithuka Kimunyi – mshukiwa wa mauaji – alipokuwa kwenye Green Army. Kwa sasa, Kimunyi anazuiliwa kwa siku 14 kuhojiwa na polisi. Matanka alizikwa Jumanne nyumbani kwao Kajiado kwa mujibu wa desturi za Kiislamu. Inaaminika kuwa Matanka na Kimunyi walianza urafiki wa karibu, licha ya tofauti ya umri – Kimunyi akiwa na miaka 56, mara mbili ya umri wa Matanka. Katika mojawapo ya mazungumzo kati ya Rais na wanachama wa Green Army , aliwauliza kama kuna yeyote aliyekuwa na hamu ya kujiunga na Huduma ya Kitaifa ya Polisi. Matanka alikuwa mmoja wa wale waliotangaza nia kwa kuinua mkono wake kwa ujasiri. Ndipo alipopata nafasi ya kujiunga moja kwa moja na Kikosi cha GSU. Hatimaye, aliteuliwa kujiunga na kikosi maalum kinachotoa ulinzi Ikulu na makazi ya Rais kote nchini. Mnamo Julai 2025, Matanka alihamishiwa Ikulu ya Nairobi kama afisa wa ulinzi chini ya utawala wa Rais wa sasa, Dkt William Ruto. Kazi yake ilikuwa kuchunguza wageni na magari yanayoingia kupitia malango mbalimbali ya Ikulu. Alikuwa mstari wa kwanza wa ulinzi endapo kungetokea tishio lolote la usalama. Wakati Matanka alirejea Ikulu kama afisa wa GSU, mkataba wa Kimunyi ulikuwa umeisha. Lakini urafiki wao uliendelea. Mara kwa mara, Matanka na Kimunyi walikutana katika milango tofauti ya Ikulu kulingana na ni lango lipi Matanka alikuwa akilinda siku hiyo. Polisi sasa wanadai kuwa Jumatatu, Kimunyi alificha mshale kwenye gunia na aliingia katika kibanda cha ulinzi cha Lango D la Ikulu, na kumpiga Matanka kwa mshale kifuani hadi kumuua. Maafisa wawili wenzake Matanka waliokuwa wakikagua gari wakati tukio lilipotokea, wametoa taarifa kwa DCI. Wameeleza kuwa urafiki kati ya Matanka na Kimunyi ulikuwa wa wazi, na hata waliruhusiwa kuketi pamoja ndani ya kibanda cha ulinzi jambo ambalo kawaida ni kosa la kiusalama. Afisa mmoja anayehusishwa na uchunguzi alieleza kuwa picha za CCTV, ambazo sasa zinachunguzwa na DCI wa Kilimani, zilionyesha mazungumzo kati ya Matanka na Kimunyi yalidumu kwa takriban dakika 17 kabla ya tukio. “Baada ya kuangalia CCTV, tunasema wazi kulikuwa na uzembe mkubwa kwa upande wa maafisa,” alisema mpelelezi huyo. Katika video hiyo, inaonyeshwa kuwa maafisa wenzake waliondoka wakimuacha Matanka akiendelea kuzungumza na Kimunyi. Ndipo mshukiwa alichomoa mshale na kumdunga Matanka, ambaye alianguka chini. Uchunguzi huu ni tofauti na taarifa ya awali ya Huduma ya Polisi, ambayo ilisema kwamba mtu mwenye silaha aliyekuwa akizurura alifyatua mshale baada ya kuonywa na maafisa wa usalama. Kimunyi sasa anazuiliwa kwa siku 14 kwa agizo la mahakama ya Nairobi, wakati uchunguzi unaendelea. Afisa mmoja wa DCI aliliambia gazeti la Taifa Leo kuwa Kimunyi bado hajatoa maelezo kamili ya mauaji hayo, na badala yake anadai kuwa alichochewa na “nguvu za giza”. Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja alisema hawezi kutoa taarifa kwa sasa hadi uchunguzi utakapokamilika: “Tusubiri uchunguzi ukamilike ndipo tuelewe kilichotokea,” alisema kwa njia ya simu. Wakati huohuo, Kamanda wa GSU Robinson Lolomodon amewaagiza maafisa wa juu wa polisi wanaolinda Ikulu kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Detectives Arrest Two in Sh720 Million Gold Scam Targeting American Businesswoman

Detectives Arrest Two in Sh720 Million Gold Scam Targeting American Businesswoman

Detectives have arrested two men linked to a Sh720 million ($5.6 million) gold scam that targeted an American businesswoman in Nairobi. The suspects — identified as Michael Otieno Onyango and Andrew Clifford Otieno — were nabbed following a sting operation by officers from the Directorate of Criminal Investigations (DCI). According to a statement released by [...] The post Detectives Arrest Two in Sh720 Million Gold Scam Targeting American Businesswoman appeared first on Kahawatungu .

Cherargei questions Harambee Stars’ winning mentality without financial incentives

Cherargei questions Harambee Stars’ winning mentality without financial incentives

Nandi Senator Samson Cherargei has raised concerns over the Harambee Stars’ performance following Kenya’s 3-0 defeat to Ivory Coast in Abidjan on Tuesday, October 14, 2025. In a post on X dated October 15, Cherargei questioned the team’s motivation and reliance on incentives, stating, “Yaani, you mean Harambee Stars cannot win without financial/money enticement? Or […]

Anayeshukiwa kuua afisa Ikulu azuiliwa kubaini alivyobeba silaha licha ya ulinzi mkali

Anayeshukiwa kuua afisa Ikulu azuiliwa kubaini alivyobeba silaha licha ya ulinzi mkali

MWANAMUME anayeshukiwa kumuua kwa mshale afisa wa kikosi maalum cha ulinzi wa Rais karibu na Ikulu ya Nairobi siku ya Jumatatu, atazuiliwa na polisi kwa kipindi cha siku 14 huku uchunguzi ukiendelea, mahakama imeamuru. Kithuka Kimunyi Musyimi, mwenye umri wa miaka 56, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kibera, Bi Christine Njagi, ambapo aliagizwa azuiliwe korokoroni katika Kituo cha Polisi cha Kilimani. Akiwa korokoroni, Musyimi atahojiwa kwa kina na maafisa kutoka Kitengo cha Uhalifu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI). Mchunguzi wa kesi hiyo, Inspekta Bashir Boya, alimweleza hakimu kuwa polisi wanahitaji muda wa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo Musyimi alishirikiana na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, pamoja na sababu ya kufika eneo kama Ikulu akiwa amejihami kwa silaha. "Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa afisa aliyeuawa, Ramadhan Matanka, ambaye alikuwa mwanachama wa kikosi cha GSU kinacholinda Rais, alikuwa kazini katika Lango D la Ikulu wakati mshukiwa alimvamia akiwa na upinde na mshale aliouficha kwenye gunia," alisema Inspekta Boya. Kwa mujibu wa maelezo ya Inspekta huyo, mshukiwa alijificha nyuma ya gari lililokuwa linakaguliwa, akatoa mshale kutoka kwenye gunia na kumpiga Konstebo Matanka kifuani upande wa kushoto, akimsababishia majeraha mabaya. Mahakama iliambiwa kuwa mshukiwa hana makazi yanayojulikana wala kazi rasmi, na kwa hivyo ni hatari kuachiliwa kwa dhamana kwani anaweza kutoroka na kuhujumu uchunguzi. “Tuna hofu kuwa akiachiliwa kwa dhamana, anaweza kutoweka,” alisema Inspekta Boya. Mahakama iliambiwa kuwa uchunguzi umegawanywa katika maeneo matano, ikiwemo kurekodi taarifa za mashahidi, kukagua picha za kamera za CCTV katika Lango D na barabara ya Dennis Pritt, kuchambua mawasiliano ya simu ya mshukiwa, kuchukua alama za vidole na kuziwasilisha kwa kitengo cha kumbukumbu za uhalifu, kumpima hali yake ya akili kabla ya kushtakiwa kwa kosa la mauaji. Inspekta Boya alieleza kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi, faili itawasilishwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) apitie ushahidi na kutoa mwongozo kuhusu mashtaka atakayofunguliwa mshukiwa. Marehemu Matanka alizikwa jana katika kaunti ya Kajiado. Musyimi, ambaye alionekana kutembea kwa shida na kusaidiwa na maafisa wawili wa polisi, aliomba apelekwe hospitalini akidai alipigwa baada ya tukio hilo. Alipoulizwa kama alipinga ombi la polisi kumzuilia kwa siku 14, Musyimi hakupinga. Katika uamuzi wake mfupi, Hakimu Njagi alisema polisi wamewasilisha sababu za msingi za kuendelea kumzuilia mshukiwa. “Nimepitia ombi na hati ya kiapo ya kuunga kuzuiliwa kwa mshukiwa kwa siku 14. Nimeridhika kuna sababu za msingi. Ombi hili lina mashiko,” alisema Bi Njagi. Mahakama pia iliagiza mshukiwa kupelekwa hospitalini kupata matibabu na kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 28 2025 ili upande wa mashtaka utoe taarifa kuhusu hali ya uchunguzi.