Raila Odinga’s Body Arrives at Jomo Kenyatta Stadium in Kisumu for Public Viewing

Raila Odinga’s Body Arrives at Jomo Kenyatta Stadium in Kisumu for Public Viewing

The body of former Prime Minister Raila Odinga has arrived at the Jomo Kenyatta International Stadium in Mamboleo, Kisumu, for public viewing, marking a solemn moment in Kenya’s national mourning. The body was airlifted from Kisumu International Airport to the stadium, a move that caught many of his supporters by surprise. Thousands had camped at [...] The post Raila Odinga’s Body Arrives at Jomo Kenyatta Stadium in Kisumu for Public Viewing appeared first on Kahawatungu .

Kama sio Raila, serikali yangu ingeporomoka, afichua Ruto

Kama sio Raila, serikali yangu ingeporomoka, afichua Ruto

Rais William Ruto, jana alitoa ushuhuda wa kipekee na wa kugusa moyo kuhusu mchango mkubwa wa Raila Odinga katika kuokoa taifa wakati wa maandamano makubwa ya vijana wa kizazi cha Gen Z mnamo mwaka 2024. Akihutubia taifa wakati wa ibada ya kitaifa ya wafu ya Waziri Mkuu huyo wa zamani katika Uwanja wa Nyayo, Rais Ruto alikiri kwa mara ya kwanza hadharani kwamba serikali yake ilinusurika kuporomoka kwa sababu ya  usaidizi wa Raila Odinga ambaye alikuwa mpinzani wake wa muda mrefu. “Tulikuwa tumeshirikiana awali katika Pentagon, tukaja kuwa wapinzani. Lakini mwaka jana, njia zetu zilikutana tena,  safari hii si kwa ushindani, bali kwa ajili ya kuokoa taifa,” alisema Ruto kwa hisia nzito. Rais alirejelea miezi ya maandamano katikati ya mwaka 2024 ambapo maelfu ya vijana walimiminika barabarani wakipinga ufisadi, gharama ya juu ya maisha, na ukosefu wa uwajibikaji serikalini. Maandamano hayo yaliyopangwa  mitandaoni yalitikisa misingi ya utawala wa  Kenya Kwanza. Katika hali  ambayo haibainika wakati huo, Raila alichukua nafasi ya mpatanishi kimya kimya, na akasaidia kuweka msingi wa serikali jumuishi. Rais mwenyewe alithibitisha hilo hadharani jana. Kupitia ushawishi wa Raila, wafuasi wake waaminifu waliteuliwa kushikilia nyadhifa muhimu serikalini. John Mbadi aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, Hassan Joho waziri wa madini, Opiyo Wandayi kuwa Waziri wa Kawi, Wycliffe Oparanya kuwa Waziri wa Ushirika, huku Beatrice Askul akiongoza Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais alisema hakuzungumza kama mshindi wa kisiasa, bali kama mtu aliyenusurika na kusaidiwa na mtu aliyekuwa mpinzani wake wa muda mrefu. “Tulikuwa washirika na wapinzani, marafiki na mahasimu, lakini daima tulikuwa wazalendo,” alisema, akimkumbuka Raila kama “mpatanishi, mzalendo, na dira ya maadili.” Akimtaja Raila kama “jasiri, mwenye nguvu thabiti na moyo usioyumba,” Rais Ruto alisisitiza kuwa “historia itamhukumu Raila kwa haki na kwa wema.” Kwa sauti iliyojaa hisia, alihitimisha hotuba yake kwa kuimba ubeti wa wimbo wa Raila alioupenda — Jamaica Farewell , akisema: “Kwa wimbo huu, tunakushukuru, Baba, kwa kila hatua uliyopiga kwa ajili yetu sote.” Rais alitambua kuwa katika kujenga taifa, si lazima wote wakubaliane kisiasa, bali kila mmoja ana nafasi ya kuhudumu kwa manufaa ya Kenya. Aidha, alisisitiza kuwa urithi wa Raila hautapimwa kwa vyeo alivyowahi kushikilia, bali kwa mchango wake kwa taifa: kupigania demokrasia, kushinikiza mageuzi ya katiba,na kusimama na wale waliotengwa na mfumo wa utawala. “Katika kila changamoto tuliyokutana nayo, Raila alionyesha kwamba kuwa mpinzani wa serikali si kuwa adui wa nchi. Ni kuwa mlinzi wa misingi ya haki na maadili,” alisema Rais. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alitoa heshima za kipekee kwa Raila Odinga akimtaja kama mzalendo wa kweli na mtu aliyefanikisha historia ya taifa. “Raila aliipenda Kenya kuliko kitu kingine chochote. Alikuwa baba kwa wote, hakuwahi kuwa na ukabila, na aliwapenda Wakenya wote kwa usawa,” alisema Rais Kenyatta, akikumbuka jinsi nyumba ya Odinga ilivyokuwa wazi kwa watu wa matabaka na makabila yote. Kauli hiyo haikuwa tu heshima ya kisiasa, bali pia ilikuwa kauli ya upatanisho binafsi kutoka kwa aliyekuwa mpinzani wake wa kisiasa kwa miaka mingi. “Historia ya Kenya haiwezi kuandikwa bila jina la Raila Odinga kuwa miongoni mwa ya kwanza,” aliongeza. “Hadithi ya demokrasia, ugatuzi, na utetezi wa haki za wananchi wa kawaida  zote zina alama yake.” Sauti ya Kenyatta ilibeba uzito wa mtu aliyeelewa gharama ya uhasama wa kisiasa, lakini pia nguvu ya maridhiano. “Raila ametutoka kimwili, lakini katika mioyo yetu na katika roho ya taifa letu, ataendelea kuishi milele,” alisema kwa sauti ya huzuni.

Raila Odinga’s Body Airlifted from Kisumu Airport to Mamboleo for Public Viewing

Raila Odinga’s Body Airlifted from Kisumu Airport to Mamboleo for Public Viewing

The body of former Prime Minister Raila Odinga has been airlifted from the Kisumu International Airport to the Jomo Kenyatta International Stadium in Mamboleo for public viewing. This development came as a surprise to many of his supporters who had camped at the airport expecting the convoy to travel by road. Raila’s body arrived in [...] The post Raila Odinga’s Body Airlifted from Kisumu Airport to Mamboleo for Public Viewing appeared first on Kahawatungu .

Oburu aligeuka “Essau” kuachia Raila arithi baba yao kisiasa

Oburu aligeuka “Essau” kuachia Raila arithi baba yao kisiasa

Seneta wa Siaya, Dkt Oburu Oginga,  aliruhusu kaka yake mdogo Raila Odinga kurithi baba yake kisiasa  na akamuunga mkono hadi kifo chake. Kwa zaidi ya miongo mitatu, Oburu alisimama imara na  Raila  kama mshauri mwaminifu, mwanamikakati wa kisiasa na nguvu kimya nyuma ys familia ya Odinga. Katika familia nyingi za Kiafrika, mzaliwa wa kwanza hushikilia mamlaka ya kifamilia, na jaribio lolote la kupokonywa nafasi hiyo huibua migogoro mikali kama hadithi ya kibiblia ya Yakobo na Esau. Lakini kwa Dkt Oginga  ambaye sasa ni Kaimu Kiongozi wa Chama cha ODM, kuwa kifungua mimba katika familia ya Jaramogi Oginga Odinga kulimaanisha jambo tofauti: alichagua uaminifu badala ya uongozi, unyenyekevu badala ya mgawanyiko. “Raila hakuwa tu kaka yangu, alikuwa rafiki yangu, rika langu, mshauri wangu, mshirika wangu wa kibiashara. Nilimheshimu kama kiongozi wangu wa kisiasa,” alisema Dkt Oginga mbele ya maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa Nyayo. Kuanzia enzi za KANU hadi mabadiliko ya vyama vingi, Dkt Oginga alibaki nyuma ya Raila, akichukua mzigo wakati hali ilikuwa mbaya, akimkinga kaka yake, na kulinda ushawishi wa kisiasa wa familia. Katika dunia ambapo siasa hugawanya familia, uaminifu wa Dkt Oginga kwa kaka yake mdogo ni nadra na wa kipekee — udugu uliopimwa kwa miongo mingi ya mapambano, nguvu na kujitolea. Alizaliwa Oktoba 15, 1943, katika kijiji cha Sakwa, Bondo, Siaya  kabla ya uhuru wa Kenya. Akiwa mwana wa kwanza wa Jaramogi, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, matarajio yalikuwa makubwa. Lakini, kama anavyosema Mzee Edwin Onyango Radier, aliyekuwa msaidizi wa Jaramogi: “Oburu alikuwa mpole, mwerevu, na mwenye hekima. Hakufuata njia ya mkwaruzano kama Jaramogi au Raila. Alikuwa mkono wa utulivu katika familia ya Odinga.” Mzee Olang’o Nyabola anaongeza: “Raila alikuwa na moto wa kisiasa, jasiri na mpambanaji. Oburu alikuwa mtulivu, mwelewa na mwenye ushawishi wa chini kwa chini. Pamoja walisaidiana vyema.” Baada ya kifo cha Jaramogi 1994, wengi walidhani Dkt Oginga angechukua usukani kisiasa katika familia. Lakini alijiondoa kwa hiari, akatangaza Raila alikuwa kiongozi bora. “Uongozi si haki ya kuzaliwa,” alisema wakati huo. “Ni suala la nani anaweza kuongoza watu kwa matumaini. Raila ana kipawa hicho, nami nitamuunga mkono milele.” Na kweli, alimsaidia Raila kwa dhati, kwa zaidi ya miongo mitatu, wakati wa kukamatwa, kupigania mageuzi, kupoteza chaguzi, na kuongoza vuguvugu la matumaini nchini Kenya. Alipokuwa Mbunge wa Bondo kwa zaidi ya miaka 20, alijulikana kwa heshima, bidii, na kujitolea kwa maendeleo ya Siaya. Alihimiza ugatuzi, usawa, na uwajibikaji, sawa na misingi ya Raila. Tangu kuzaliwa kwa ODM mwaka 2005, Dkt Oginga amekuwa mmoja wa washauri wakuu. Alifahamika kama “sauti ya busara” ndani ya chama, akiwa kiungo kati ya kizazi kipya cha vijana na wanasiasa wa kizazi cha zamani. Aliwahi kuhudumu pia kama mweka hazina wa chama na mlezi wa kisera. Kila hali ilipochacha, alikuwa na uwezo wa kutuliza  kwa hekima ya kihistoria na uzoefu wa kifamilia. Dkt Oginga pia alikuwa nguzo ya familia ya Odinga. Akiwa msemaji wa familia, mara nyingi alikuwa akitoa taarifa za afya ya Raila, hata pale wasaidizi wake waliponyamaza.

Oburu afichua uhusiano wake na Raila

Oburu afichua uhusiano wake na Raila

KWA zaidi ya nusu karne, Seneta wa Siaya, Dkt Oburu Oginga, alisimama imara kando ya kaka yake mdogo Raila Odinga, si kama mpinzani, si kama mshindani, bali kama mshauri mwaminifu, mkakati wa kisiasa na nguvu kimya nyuma ya ukoo wa Odinga. Katika familia nyingi za Kiafrika, mzaliwa wa kwanza hushikilia mamlaka ya kifamilia, na jaribio lolote la kupokonywa nafasi hiyo huibua migogoro mikali kama hadithi ya kibiblia ya Yakobo na Esau. Lakini kwa Dkt Oginga ambaye sasa ni Kaimu Kiongozi wa Chama cha ODM, kuwa kifungua mimba katika familia ya Jaramogi Oginga Odinga kulimaanisha jambo tofauti: alichagua uaminifu badala ya uongozi, unyenyekevu badala ya mgawanyiko. “Raila hakuwa tu kaka yangu, alikuwa rafiki yangu, rika langu, mshauri wangu, mshirika wangu wa kibiashara. Nilimheshimu kama kiongozi wangu wa kisiasa,” alisema Dkt Oginga mbele ya maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa Nyayo. Kuanzia enzi za KANU hadi mabadiliko ya vyama vingi, Dkt Oginga alibaki nyuma ya Raila, akichukua mzigo wakati hali ilikuwa mbaya, akimkinga kaka yake, na kulinda ushawishi wa kisiasa wa familia. Katika dunia ambapo siasa hugawanya familia, uaminifu wa Dkt Oginga kwa kaka yake mdogo ni nadra na wa kipekee — udugu uliopimwa kwa miongo mingi ya mapambano, nguvu na kujitolea. Alizaliwa Oktoba 15, 1943, katika kijiji cha Sakwa, Bondo, Siaya kabla ya uhuru wa Kenya. Akiwa mwana wa kwanza wa Jaramogi, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, matarajio yalikuwa makubwa. Lakini, kama anavyosema Mzee Edwin Onyango Radier, aliyekuwa msaidizi wa Jaramogi: “Oburu alikuwa mpole, mwerevu, na mwenye hekima. Hakufuata njia ya mkwaruzano kama Jaramogi au Raila. Alikuwa mkono wa utulivu katika familia ya Odinga.” Mzee Olang’o Nyabola anaongeza: “Raila alikuwa na moto wa kisiasa, jasiri na mpambanaji. Oburu alikuwa mtulivu, mwelewa na mwenye ushawishi wa chini kwa chini. Pamoja walisaidiana vyema.” Baada ya kifo cha Jaramogi 1994, wengi walidhani Dkt Oginga angechukua usukani kisiasa katika familia. Lakini alijiondoa kwa hiari, akatangaza Raila alikuwa kiongozi bora. “Uongozi si haki ya kuzaliwa,” alisema wakati huo. “Ni suala la nani anaweza kuongoza watu kwa matumaini. Raila ana kipawa hicho, nami nitamuunga mkono milele.” Na kweli, alimsaidia Raila kwa dhati, kwa zaidi ya miongo mitatu, wakati wa kukamatwa, kupigania mageuzi, kupoteza chaguzi, na kuongoza vuguvugu la matumaini nchini Kenya. Alipokuwa Mbunge wa Bondo kwa zaidi ya miaka 20, alijulikana kwa heshima, bidii, na kujitolea kwa maendeleo ya Siaya. Alihimiza ugatuzi, usawa, na uwajibikaji, sawa na misingi ya Raila. Tangu kuzaliwa kwa ODM mwaka 2005, Dkt Oginga amekuwa mmoja wa washauri wakuu. Alifahamika kama “sauti ya busara” ndani ya chama, akiwa kiungo kati ya kizazi kipya cha vijana na wanasiasa wa kizazi cha zamani. Aliwahi kuhudumu pia kama mweka hazina wa chama na mlezi wa kisera. Kila hali ilipochacha, alikuwa na uwezo wa kutuliza kwa hekima ya kihistoria na uzoefu wa kifamilia. Dkt Oginga pia alikuwa nguzo ya familia ya Odinga. Akiwa msemaji wa familia, mara nyingi alikuwa akitoa taarifa za afya ya Raila, hata pale wasaidizi wake waliponyamaza.