Sakaja katika kinywa cha mamba Raila akiendeleza mikakati ya kumwokoa

Sakaja katika kinywa cha mamba Raila akiendeleza mikakati ya kumwokoa

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga jana alishindwa kumwokoa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja baada ya madiwani wa Nairobi kumkaidi na kuapa kukamilisha mipango ya kumng’oa kiongozi huyo madarakani. Jana, Bw Odinga alikutana na uongozi wa Bunge la Kaunti, mkutano ambao ulikuwa wa pili ndani ya siku nne. Mkutano huo ulikuwa wa kuwarai wawashawishi wenzao waachane na mpango wa kumng’atua gavana huyo enzini. Idadi ya madiwani ambao wanataka Bw Sakaja atimuliwe nayo inaendelea kuongezeka na kufikia jana walikuwa 85 kutoka 70 mnamo Ijumaa wiki jana. Juhudi za kusitisha mchakato huo zinaonekana kugonga mwamba. Bunge la Kaunti ya Nairobi kwa sasa liko likizoni kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuanza likizo Agosti 7 ambayo itadumu hadi Septemba 23. Mnamo Ijumaa, kulikuwa na mkutano uliojaa hisia tele katika makazi ya Bw Odinga mtaani Karen, Nairobi, ambao ulihudhuriwa na Bw Sakaja na uongozi wa Bunge la Kaunti. Duru zinaarifu kuwa mkutano huo ulioanza saa nne mchana, uliendelea hadi jioni lakini hakuna suluhu iliyoafikiwa. Ilidokezwa kwamba Bw Odinga alimuunga mkono Bw Sakaja na kumwambia azingatie utoaji wa huduma kwa raia na kutimiza ahadi zake na kutoa pesa za basari na maendeleo kwa wadi mbalimbali. Bw Odinga pia alimwahidi Bw Sakaja kuwa angezungumza na viongozi wengine wa Bunge la Kaunti wiki hii ili kumwokoa. Hapo jana, Bw Odinga alikuwa na mkutano mwingine wa kumwokoa gavana huyo katika afisi za wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga, Nairobi. Mkutano huo uliojaa hisia na majibizano makali pia ulihudhuriwa na Bw Odinga, Kiongozi wa Wengi Nairobi, Peter Imwatok, Spika Ken Ng’ondi, Kiongozi wa Wengi Moses Ogeto na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Bajeti Wilfred Odalo. Uongozi huo wa Kaunti ulikashifiwa kwa kunufaika na ‘wema’ wa Bw Sakaja kisha kukosa kusikia kilio cha madiwani. Hakuna chochote kilichoafikiwa katikamkutano huo huku waliohudhuria wakidai walikuwa katika shinikizo za kumtimua Bw Sakaja kutokana na jinsi hali ilivyo kiuongozi katika Kaunti ya Nairobi. Aliyekuwa Diwani wa South C, Osman Khalif ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye Afisi ya Gavana pia alihudhuria mkutano huo pamoja na Mkuu wa Wafanyakazi David Ndung’u Njoroge. Wawili hao walikashifiwa kwa kuwazuia madiwani kumfikia Gavana. “Tuna mkutano mwingine bila Raila baada ya chakula cha mchana kisha Jumanne (leo) tutakutana na Raila,” kidokezo kikasema. Aidha, mbunge mmoja kutoka Kaunti ya Nairobi aliyekuwa akifuatilia mkutano huo aliambia Taifa Leo kuwa leo uongozi wa Kaunti utawasilisha ripoti yake kwa Raila ambapo hatima ya gavana huyo itaamuliwa. “Ripoti hiyo ndiyo itaamua mustakabali wake, hapo ndipo tutajua kama atanusurika au mpango wa kumng’atua utaendelea mbele,” akasema mbunge huyo. Kufikia jana usiku, wakati wa kuchapisha habari hizi, mkutano kati ya uongozi wa Kaunti na baadhi ya madiwani ulikuwa bado unaendelea. Inadaiwa Ijumaa iliyopita, Bw Sakaja alimtafuta mwanasiasa mkongwe wa Nairobi mwenye usuli Mlima Kenya amshawishi mbunge mmoja rafiki mkubwa wa Raila. Mbunge huyo alitwikwa jukumu la kuwasilisha kilio cha Bw Sakaja kwa Raila. Kwa mujibu wa sheria za Bunge la Kaunti ni thuluthi tu ya saini inayohitajika ndipo hoja ya kumng’atua gavana mamlakani. Idadi hiyo ni saini 41 kati ya madiwani 123 ikizingatiwa diwani mmoja, Joel Muneve ambaye alikuwa diwani wa Kariobangi Kaskazini alifariki mnamo Aprili. Hata hivyo, notisi ya kuitisha kikao cha kujadili hoja ya kumtimua gavana lazima itoke kwa Spika baada ya kupokea mawasiliano kutoka kwa afisi ya upande wa Wengi au Wachache. Madiwani mbalimbali waliohojiwa walisema kuwa safari ya Bw Sakaja imefikia mwisho na wako tayari kumng’atua. Baadhi ya madiwani walioongea na Taifa Leo na kusema wako radhi kuhakikisha Bw Sakaja anaenda nyumbani ni Naibu Kiongozi wa Wachache Waithira Chege, Robert Alai (Kileleshwa), Sospeter Mumbi (Roysambu), Maurice Ochieng’ (Mountain View) na Geoffrey Majiwa (Baba Dogo) miongoni mwa wengine.

KRA marks 30 years with push for digital tax collection

KRA marks 30 years with push for digital tax collection

The Kenya Revenue Authority (KRA) has announced fresh plans to use technology to simplify tax processes and bring more Kenyans into the tax net. Speaking on Monday, September 1, 2025, during celebrations to mark the authority’s 30th anniversary, Commissioner General Humphrey Wattanga said billions have been set aside to support the move. The reforms will […]

Govt to regulate miraa trade through cooperatives

Govt to regulate miraa trade through cooperatives

The government has announced plans to streamline the miraa trade by bringing farmers and traders under cooperative societies. According to Cooperatives Principal Secretary Patrick Kilemi, the initiative is aimed at curbing theft, improving accountability, and enhancing the tracking of vehicles transporting the crop across the country. Speaking during a forum in Mombasa on Monday, September […]

Ruku reveals plan to end repeated fingerprint requirement for clearance certificates

Ruku reveals plan to end repeated fingerprint requirement for clearance certificates

Public Service Cabinet Secretary Geoffrey Ruku has revealed that the government is exploring ways to streamline the process of obtaining police clearance and good conduct certificates by ending the repeated fingerprint requirement. Speaking during an interview, on Monday night, September 1, 2025, Public Service Cabinet Secretary Geoffrey Ruku said the plan falls under a broader sector transformation […]

Meta to stop its AI chatbots from talking to teens about suicide

Meta to stop its AI chatbots from talking to teens about suicide

Meta said it will introduce more guardrails to its artificial intelligence (AI) chatbots – including blocking them from talking to teens about suicide, self-harm and eating disorders. It comes two weeks after a US senator launched an investigation into the tech giant after notes in a leaked internal document suggested its AI products could have [...] The post Meta to stop its AI chatbots from talking to teens about suicide appeared first on Kahawatungu .

Nigeria secessionist activist jailed for terrorism in Finland

Nigeria secessionist activist jailed for terrorism in Finland

A court in Finland sentenced a controversial leader of a Nigerian secessionist movement to six years in prison after convicting him of terrorism-related offences. Simon Ekpa, a Finnish citizen of Nigerian origin, “attempted to promote the independence of the so-called Biafra region in south-eastern Nigeria by illegal means”, according to court documents made available to [...] The post Nigeria secessionist activist jailed for terrorism in Finland appeared first on Kahawatungu .

Mob burns Nigerian woman to death for alleged blasphemy

Mob burns Nigerian woman to death for alleged blasphemy

A woman was burnt to death by a mob in northern Nigeria’s Niger state after she was accused of blaspheming the Prophet Muhammad, police have said. Police condemned the killing of the woman – identified in local media as a food vendor named Amaye – as “jungle justice”, saying that an investigation was under way [...] The post Mob burns Nigerian woman to death for alleged blasphemy appeared first on Kahawatungu .

Trump defends U-turn on Chinese student visas after Maga backlash

Trump defends U-turn on Chinese student visas after Maga backlash

US President Donald Trump has defended his decision to issue 600,000 Chinese student visas, despite a backlash from some supporters. He told the Daily Caller on Sunday that it would be “insulting” to ban them, and said his move would benefit smaller universities. The president is reversing the hard line his administration has taken on [...] The post Trump defends U-turn on Chinese student visas after Maga backlash appeared first on Kahawatungu .

India’s Modi has ‘insightful’ talks in Putin’s limo

India’s Modi has ‘insightful’ talks in Putin’s limo

India’s Prime Minister, Narendra Modi, says he has had an “insightful” exchange with Russian President Vladimir Putin on the sidelines of a summit in China. The two leaders spent 45 minutes inside the Russian leader’s car – after which Modi posted a picture of their journey alongside the compliment to Putin. “They were at home… [...] The post India’s Modi has ‘insightful’ talks in Putin’s limo appeared first on Kahawatungu .