Moses Kuria raises concerns over Nairobi County govt and national govt partnership plan

Moses Kuria raises concerns over Nairobi County govt and national govt partnership plan

Former Trade and Industrialisation Cabinet Secretary Moses Kuria has expressed concern over the looming takeover of key functions of the Nairobi County by the national government. Taking to X on Tuesday, October 14, 2025, Kuria linked the problems bedevilling the country’s capital city, such as poor lighting and the garbage menace, to former governments’ interferences. […]

AFC Leopards confirm venue change against Bandari

AFC Leopards confirm venue change against Bandari

AFC Leopards have confirmed that their third outing of the 2025/2026 Kenyan Premier League season against Bandari FC will be staged at the Moi International Sports Centre, Kasarani, on Wednesday, October 15, 2025, and not at Nyayo National Stadium as earlier communicated. Meanwhile, the Football Kenya Federation and league organisers have released the final fixtures […]

Ni sisi tuko! Cape Verde wafuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa

Ni sisi tuko! Cape Verde wafuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa

KOCHA Pedro Brito wa timu ya taifa ya Cape Verde amesema kikosi chake kiko tayari kupambana na miamba nchini Amerika mwaka ujao, baada yao kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa. Wanavisiwa wa Cape Verde waliweka historia ya kuwa nchi ndogo ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia, ushindi ambao umifanya kuwa nchi ya pili katika historia kufuzu kwa mashindano hayo makubwa zaidi duniani. Kuelekea mechi za jana usiku, mataifa ya bara Afrika ambayo yalikuwa tayari yamefuzu ni Algeria, Cape Verde, Egypt, Ghana, Morocco na Tunisia. Nafasi zingine nne zilikuwa ziamuliwe katika mechi za jana usiku, kufikisha jumla ya mataifa tisa ya Afrika yatakayonogesha kindumbwendumbwe hicho cha mwaka ujao. Kombe la Dunia 2026 litashirikisha timu 48 na litaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Amerika, Canada na Mexico. Awamu ya kwanza ya mchujo wa mataifa ya bara Afrika ulikamilika jana usiku huku washindi wa makundi tisa wakijikatia tikiti ya moja kwa moja. Timu zitakazomaliza nambari mbili katika kila kundi zitapigwa tathmini li kubaini nne bora miongoni mwao. Ni hizo zitakazoingia katika droo ya awamu ya pili ya mchujo, ambapo mshindi atawakilisha Afrika katika mchujo baina ya mabara mwaka ujao. Kikosi hicho cha kocha Pedro Brito kilifuzu kwa kipute hicho kitakachofanyika kwa wakati mmoja nchini Amerika, Mexico na Canada baada ya kutandika Eswatini 3-0 kwenye mechi ya mwisho ya Kundi D iliyosakatiwa Jumatau. Timu zingine kutoka Afrika zilizokuwa zimefuzu kwa fainali hizo kufikia jana kabla ya kwenda mitamboni ni 2026 ni Morocco, Tunisia, Misri, Algeria na Ghana. Baada ya kutofungana katika kipindi cha kwanza, Cape Verde maarufu kama Blue Sharks walirudi uwanjani wakiwa na ari na kupata mabao hayo kupitia kwa nahodha Dailon Livramento kabla ya Willy Semedo na Tavares Stopira kuongeza mawili. Kutoka jijini hapa (Praia) hadi visiwa vya Sao Vicente na Sal, wananchi wa taifa hili la Afrika Magharibi walijitokeza kwa wingi barabarani kufurahia ushindi huo baada ya mwamuzi kupuliza firimbi ya kumaliza mchezo. "Tumeota ndoto hii kwa miaka mingi, Ushindi huu ni kwa ajili ya kila mwananchi ya taifa hili aliye hapa nchini ya nje. Hii ni ndoto iliyotimia. Soka imetuleta pamoja kama taifa," alisema Livramento baada ya mechi hiyo iliyochezewa Esadio Nacional de Cabo Verde. Baada ya kumaliza mechi zake 10 za kundi, Cape Verde wamemaliza kileleni na pointi 23, baada ya kushinda mara saba, kutoka sare mara mbili na kushindwa mara moja pekee, matokeo ambayo yameshangaza mashabiki wengi Duniani. Baada ya kutoka sare 3-3 na Libya, ilikuwa lazima washinde Eswatini ili kufuzu moja kwa moja. Brito ambaye amekuwa na timu hiyo tangu 2021 alisema ndoto yao ilitimia kutokana na nidhamu na umoja wa wachezaji. "Sisi ni taifa ndogo lakini umoja wetu ni mkubwa. Timu ilijiamini na timefaulu baada ya safari ndefu. Kufuzu ni mwanzo tu. Tunataka kwenda huko kupambana, wala si kushiriki tu," alisema Brito baada ya mechi hiyo iliyohudhuriwa na zaidi ya mashabiki 15,000. Kwa ufanisi huo, Cape Verde ambayo ni nchini ya watu wapatao 600,000 imejiunga na Iceland ambayo ndiyo nchi ndogo pekee iliyoandika historia kama hiyo. Mara tu baada ya mechi kuamlizika, magari yalipiga honi, huku miziki ikizikika kwa sauti ya juu kote mitaani. Rais Jose Maria Neves aliungana na wananchi kufurahia ushindi huo wa kihistoria huku akitumia wakati huo kutuma ujumbe wa pongezi kwa wachezaji, akiutaja ushindi huo kuwa wa imani, uvumilivu na umoja wa taifa zima. Cape Verde imeonyesha ulimwengu kuwa hata mataifa madogo yanaweza kutimiza ndoto kubwa," Maria Neves aliandika kwenye ukurania wake wa kijamii. Akizungmza kuhusu kufuzu huko wa historia, Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe alisema litakuwa somo kwa mataifa mengine madogo kwamba bidii na umoha vinaweza kuzaa matunda. Kocha Brito alisema timu yake itaanza kushiriki mechi za kirafiki mwishoni mwa mwaka huu ka lengo la kuimarika kabla ya fainali hizo za Kombe la Dunia. Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumatatu Equatorial Guinea 1-1 Liberia, Sao Tome and Principe 1-0 Malawi, Mauritius 0-0 Libya, Loseotho 1-0 Zimbabwe, Cameroon 0-0 Angola, Cape Verde 3-0 Eswatini.