Pazia lafungwa watiania urais Zanzibar

Pazia lafungwa watiania urais Zanzibar

Unguja. Pazia la uchukuaji wa fomu za kuwania urais wa Zanzibar kupitia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) limefungwa rasmi leo, Jumatatu, Septemba 1, 2025, baada ya vyama vyote 17 vilivyoomba kushiriki katika kinyang’anyiro hicho kukamilisha mchakato huo. Mchakato huo ulianza Agosti 30, 2025, na wagombea kutoka vyama sita walichukua fomu siku hiyo, wengine sita wakachukua Agosti 31, na leo Jumatatu, Septemba mosi, 2025, vyama vitano vimekamilisha hatua hiyo, hivyo kufunga rasmi kazi hiyo. Vyama vilivyofunga pazia kwa leo ni pamoja na Chama cha United Democratic Party (UDP), Chama cha Makini, United Peoples Democratic Party (UPDP), Alliance for Democratic Change (ADC) na Democratic Party (DP). Kwa mujibu wa ratiba ya ZEC, uchukuaji wa fomu za uteuzi wa urais, uwakilishi na udiwani ulianza Agosti 28 na utahitimishwa Septemba 10, 2025, kabla ya uteuzi wa wagombea rasmi kufanyika Septemba 11, siku ambayo kampeni pia zitaanza. Akizungumza wakati wa kukabidhi fomu hizo, Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi, amewataka wagombea kuwa makini katika kujaza fomu na kuhakikisha wanazingatia muda wa kurejesha, ambao ni kabla ya Septemba 10, saa 10 jioni. Hata hivyo, amewashauri kurudisha mapema ili tume izihakiki kwa ufanisi kabla ya siku ya uteuzi. Mgombea urais kupitia UDP, Neema Salim Hamad, akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu, ameahidi endapo atapitishwa na kupata ridhaa ya wananchi, atapigania haki za wanawake na watu wenye ulemavu. Ametaja vipaumbele vyake vingine kuwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya, maji safi na salama pamoja na elimu, huku akisisitiza kuwa changamoto hizo zinawaathiri moja kwa moja wanawake. Aidha, amewataka wanawake kuondoa woga na kutambua kuwa wana uwezo mkubwa wa kuchangia maendeleo ya Taifa na kupigania haki zao, hivyo wasijione wanyonge. “Iwapo nitapata urais, vipaumbele vyangu vitakuwa kushughulikia masuala ya wanawake, watu wenye ulemavu, huduma za maji, elimu na afya. Wanawake waondoe woga, wajue kwamba tunaweza, na wasimame kupigania haki zao bila kujirudisha nyuma,” amesema. Mgombea urais kupitia Chama cha Makini, Ameir Hassan Ameir, amesema endapo atachaguliwa atahakikisha kila Mzanzibari anapokea Sh500,000 kila mwezi kwa ajili ya kujikimu kimaisha. Aidha, ameahidi mshahara wa kima cha chini kwa wafanyakazi wa umma utafikia Sh1.5 milioni. “Kumekuwa na maswali mengi kuhusu fedha hizo zitatoka wapi, lakini naomba niwatoe wasiwasi. Siku ya kurejesha fomu baada ya kuteuliwa na tume nitafafanua chanzo cha fedha hizo,” amesema Ameir. Ameongeza kuwa Zanzibar kwa sasa ina kundi dogo la watu wanaoneemeka, kinyume na malengo ya Chama cha Afro Shiraz (ASP), kilichokusudia wananchi wote waishi maisha bora. “Wananchi wanapaswa kula chakula wanachokipenda, siyo kile wanacholazimishwa. Naomba Wazanzibari watuunge mkono kwa kuwa chama hiki kitaleta mageuzi makubwa,” amesema. Pamoja na hayo, Ameir ameahidi kuwatetea madereva wa daladala na bodaboda, akionya kuwa wale wanaowanyanyasa wajiandae kukabiliana na hatua kali za kisheria pindi atakaposhika madaraka. Kwa upande wake, mgombea urais kupitia Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Hamad Mohamed Ibrahim, amesema chama chake kitaleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Ameeleza kuwa mfumo mpya utakuwa na Rais, Waziri Kiongozi na Naibu Waziri Kiongozi, na Naibu Waziri Kiongozi atatoka chama cha upinzani. “Lengo letu kubwa ni kuijenga Zanzibar ya viwanda ili kuzalisha ajira kwa vijana. Tutaanzisha vinu viwili vya nyuklia, kimoja Unguja na kingine Pemba, vitakavyosaidia kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na pia kusaidia ulinzi wa nchi,” amesema Ibrahim. Ameongeza kuwa vinu hivyo vitakuwa nyenzo ya kukabiliana na changamoto za usalama na uhalifu. “Tumejipanga vizuri na wananchi wanatukubali, hivyo tuna imani na tume ya uchaguzi kwamba uchaguzi utakuwa wa haki na huru, na mshindi atatangazwa bila upendeleo. Sisi tupo miongoni mwa wanaotarajia kushika wadhifa huo,” amesema. Mgombea huyo ameahidi pia kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya sheria ili kujenga Zanzibar mpya yenye ustawi na maendeleo kwa wote. Mgombea urais kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Hamad Rashid Mohamed, amesema bado yapo maeneo muhimu yanayohitaji kushughulikiwa kwa haraka, likiwamo suala la upatikanaji wa chakula, ambapo zaidi ya asilimia 75 ya mahitaji ya Zanzibar huagizwa kutoka nje ya nchi. Amesema endapo atapitishwa na ZEC na kupata ridhaa ya wananchi, chama chake kitalifanyia kazi suala hilo kwa muda mfupi, kwa kuwa tatizo hilo linachangiwa na ukosefu wa ubunifu wa kiutendaji. Akitoa mfano wa uzoefu wake, Hamad amesema alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwaka 1982, alibaini tatizo la njaa magerezani na kumshauri Rais wa wakati huo, hayati Julius Nyerere, hatua iliyosaidia kupata suluhisho la changamoto hiyo. “Tatizo ni kwamba mara nyingi watu wanapomwendea Rais huwa wanaenda na matatizo bila kupeleka suluhisho. Zanzibar inahitaji hekta 10,000 ili kuzalisha tani 250 za mchele, na ndani ya miaka mitatu tukipewa ridhaa, tuna uwezo wa kufanikisha hilo,” amesema Hamad. Ameongeza kuwa mbali na upatikanaji wa chakula, ADC imelenga kupunguza bei ya nyama kutoka Sh15,000 hadi Sh7,000 kwa kilo moja. “Iwapo wakulima na wavuvi wakipewa vifaa bure na mafunzo ndani ya mwaka mmoja bila masharti ya kukopa, ninaamini Wazanzibari watakula vizuri na kupata maisha bora,” amesema. Hamad amesema kufanikisha hayo kutahitaji Dola milioni 100 za Marekani, fedha ambazo zinaweza kupatikana kwa urahisi kupitia mapato ya sekta ya utalii endapo zitasimamiwa vizuri na kuelekezwa moja kwa moja kwa wakulima na wavuvi. Pia ameahidi kuimarisha kilimo cha karafuu na mwani ili wakulima wanufaike ipasavyo. Naye mgombea urais kupitia Chama cha Democratic Party (DP), Shaffii Hassan Suleiman, amesema kipaumbele cha kwanza iwapo watapata madaraka ni kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa, kwa kuwa bila amani hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa. Amesema chama chake kitalenga pia kutoa ajira kwa kila Mzanzibari, hususan vijana ambao kwa sasa wengi wao wanahangaika mitaani bila kipato. “Kama mkulima, nafahamu changamoto wanazopitia wakulima wenzangu. Kwa sasa hakuna viwanda vya kusindika mazao, hivyo kazi kubwa ya chama chetu itakuwa ni kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji wa viwanda na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinapata masoko nje ya nchi,” amesema Shaffii. Ameongeza kuwa chama chake kitalenga kuongeza masoko ya ndani na nje ya nchi, pamoja na kujenga viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao na kuzalisha ajira zaidi. Mweyekiti ZEC Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi, amesema vyama vyote 17 vimechukua fomu za kuomba kutia nia ya kuwania kiti cha urais Zanzibar. “Kazi yetu imekwenda vizuri na leo tumemaliza kutoa fomu kwa vyama 17 vilivyoleta barua. Tunachosubiri sasa ni kurejeshwa kwa fomu hizo ili utaratibu mwingine uendelee kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni Septemba 11, 2025,” amesema Jaji Kazi.

Mbio za Meru Pazuri kusaidia watoto njiti

Mbio za Meru Pazuri kusaidia watoto njiti

ARUSHA: MBIO za Meru Pazuri maalumu kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa njiti zitafanyika Septemba 21, 2025 wilayani Arumeru mkoani Arusha. Zikijulikana kama ‘Meru Pazuri Afya Marathon and Festival ‘ zitahusisha kilometa 21,kilimeta 10 na kilometa 5 zimeandaliwa na wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Meru ambapo mbali na kulenga kuchangia vifaa kwa watoto wanaozaliwa … The post Mbio za Meru Pazuri kusaidia watoto njiti first appeared on HabariLeo .

Msongamano wa wagonjwa wapungua hospitali wilaya ya Geita

Msongamano wa wagonjwa wapungua hospitali wilaya ya Geita

GEITA: HALMASHAURI ya Wilaya ya Geita mkoani Geita imepokea na kutumia kiasi cha fedha sh 893.43 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Geita. Kaimu Mganga Mfawidhi na Mfamasia wa Hospitali hiyo, Dk Simon Kalumanga ameeleza hayo Septemba 01, 2025 wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa … The post Msongamano wa wagonjwa wapungua hospitali wilaya ya Geita first appeared on HabariLeo .

Africa’s food future lies in the hands of its young entrepreneurs

Africa’s food future lies in the hands of its young entrepreneurs

Ending hunger in Africa is not about growing more maize or producing more milk. It demands a balance that involves scaling agronomic solutions such as fertilizer, improved seeds, and irrigation, while mobilizing young people to deliver the systems that make these tools work. Fertilizer, for example, only works when it reaches farmers at the right … The post Africa’s food future lies in the hands of its young entrepreneurs first appeared on Daily News .

Kizimkazi residents hail the Zanzibar government for free medical services

Kizimkazi residents hail the Zanzibar government for free medical services

ZANZIBAR: RESIDENTS of Kizimkazi Mkunguni in Zanzibar have expressed pride and joy over the completion of a modern health centre built to hospital standards, which provides free medical services to all members of the public. The health centre was officially inaugurated on January 3, 2025, by former President of Tanzania’s Fourth Phase Government, Dr. Jakaya … The post Kizimkazi residents hail the Zanzibar government for free medical services first appeared on Daily News .